UCHUNGUZI WA UUNDAJI WA VITAMBULISHO VYA UTAIFA KATIKA TAMTHILIA YA MSTAHIKI MEYA

Authors

  • Margaret June Achieng` Mung`ala
  • George Obara Nyandoro
  • Charles Nyandoro Moochi

DOI:

https://doi.org/10.47672/ajep.560
Abstract views: 331
PDF downloads: 365

Abstract

Utafiti huu ulichunguza uundaji wa vitambulisho vya utaifa katika tamthilia ya Mstahiki Meya, Arege (2009).Tamthilia ni kazi ya kidrama na ya kimaongezi ambayo huigizwa mbele ya hadhira au ni kazi iliyoandikwa ili kusomwa na hadhira. Isitoshe maagizo haya huakisi hali halisi katika jamii. Lengo kuu la kutunga tamthilia ni kuadilisha na kuwawezesha wananchi kutambua baadhi ya mambo yanayotendeka katika jamii halisi kwa kuwa, fasihi ni ukweli wa maisha. Vitambulisho ni sifa, hisia ama imani ambazo humtofautisha mtu au kabila au raia wa nchi fulani na nyingine. Huku utaifa ni hali ambapo wananchi wote hujitambua kuwa sawa katika taifa fulani na hushiriki kwa pamoja katika kuleta amani na maendeleo taifani mwao.Utafiti huu ulinuia kujibu swali lifuatalo, Kwanza, dhana ya vitambulisho vya utaifa vimejitokezaje kwa mujibu wa tamthilia ya Mstahiki Meya? Utafiti huu uliongozwa na nadharia ya uhistoria mpya ikishirikiana na nadharia ya utaifa. Umuhimu wa utafiti huu ni kwamba, utaongeza maarifa katika nadharia na mbinu za uhakiki wa tamthilia za Kiswahili nchini Kenya, kwa kurejelea na kuweka wazi vitambulisho vya utaifa, pia utaweza kutumika katika taaluma ya fasihi hususan tamthilia, kama marejeleo na itawasaidia wanafunzi na watafiti watakaotaka marejeo ya tamthilia ya Kiswahili nchini Kenya ili kuweka wazi vitambulisho vya utaifa na jinsi vinavyojitokeza  katika tamthilia, vilevile ni malighafi kwani utatoa mchango mkubwa katika historia ya tamthilia nchini Kenya na kutajirisha maktaba ya chuo kikuu cha Kisii. Aidha, tume ya utangamano wa taifa nchini Kenya (NCIC), itagundua umuhimu wa fasihi kupitia tamthilia, katika uundaji wa vitambulisho vya utaifa inayoendeleza utangamano nchini hivyo basi itawawezesha kufadhili tafiti zitakazonuia kushughulikia suala hili. Uchunguzi huu ulifanywa maktabani. Muundo wa utafiti uliotumiwa ni utafiti elezi. Kwa hivyo matokeo yaliwasilishwa kupitia maelezo

Downloads

Download data is not yet available.

Author Biographies

Margaret June Achieng` Mung`ala

Idara ya Lugha, Isimu Na Fasihi

Chuo Kikuu Cha Kisii, Kenya

George Obara Nyandoro

Idara ya Lugha, Isimu Na Fasihi

Chuo Kikuu Cha Kisii, Kenya

Charles Nyandoro Moochi

Idara ya Mtaala, Ufundishaji Na Nyenzo za Kufundishia

Chuo Kikuu Cha Kisii, Kenya

References

Alice, N .Taming the Demon of Kenya’s Election Violence:A Strategy for the NCIC Nov 4. 2011

Alter, P. (1994). Nationalism. Bristol: J.W Arrow Smith Ltd.

Amali, I. .. (2013). Cultural Pluralism. Reconstructive education and nation building in Nigeria .

Anderson, B. (2006). Imagined Communities Relections on the Origin and spread of Nationalism. Edinburgh: Quebecor World,Fairfield.

Arege, T. (2007). Kielezi Cha Tungo. Nairobi: Focus.

Babbie, R. (2010). The Practice of Social Research. Belmont: Wadsworth Centage Learninig.

Bertoncini. (2009). Outline of Swahili literature. Leiden: Boston brill.

Breuilly, J. (1993). Nationalism and the State,2nd Ed. manchester: Manchester university press.

Chimera, R. (2000). Kiswahili:Past,Present and future. Nairobi: NRB.University Press.

D. Njengere. (march 2014). Role of Curriculum in Fostering national Cohesion and Integration. Geneva: UNESCO International bureau of education.

Elimu, W. y. (2007). Secondary school kiswahili syllabus. Nairobi: k.i.e.

Eriksen, T. (2002). Anthropological Perspective. Ethnicity and Nationalism .

Flick, U. (2009). An Introduction to Qualitative Research 4th. ed. New Delhi: Sage.

Ghurye, G. (1968). Social Tension in India. Bombay: Prakasha.

Hariyanna, M. (1995). The Essentials of India philosophy. New Delhi: Motilal.B.

Harrow, K. W. (2001). Research in African Literatures. Nationalism , volume 32,number 3.

Jega, A. (2002). Education,Democracy and Nation Building in Nigeria in the 21st century. African symposium .

John.N, C. (2009). Qualitative,Quantitative and Mixed Approaches. Nebraska: Sage.

Joseph, L. R. (1999). Recent Theories of Nationalism .

Joseph, L. R. (1999). Recent Nationalism theories .

K.W.Wamitila. (2008). Kichocheo Cha Fasihi Simulizi na Fasihi Andishi. Nairobi: Phoenix.

K.W.Wamitila. (2002). Uhakiki wa Fasihi:Msingi na Vipengele Vyake. Nairobi: Phoenix Publishers Ltd.

Khahn, J. .. (2004). Research in Education. New Delhi: Prentice hall of India.

Kochhar, S. (1991). The Teacchings of social studies. New Delhi: Sterling.

Kochhar, S. (1991). The teachings of social studies. New Delhi: Sterling Private limited.

Kombo, D. &. (2006). Proposal and Thesis Writing.2nd ed vol .1. Nairobi: Paulines P.Africa.

L.T. Muliro, E. ,. (2012). History and Goverment. Nairobi: Longman.

Leinwand, G. (1992). Public Education :American Issues. UK: Roundhouse.

Longhorn. (2011). Kamusi ya karne ya 21. Nairobi: English press ltd.

Manual, T. C. Guidelines for preparations and Submissions of Thesis and Dissertations.

Mayring, P. (2004). Qualitative Content Analysis. New Delhi: Sage

Milibrand, Ralph (1969), Theory of the State - Instrumentalist and Structuralism

Mohammed, S. A. (1995). Kunga za Nathari za Kiswahili:Riwaya,Tamthilia na Hadithi fupi. EAEP.

Mohammed, S. (2000). Kitumbua kimeingia Mchanga. Nairobi: Oxford university press.

Moorman, M. (2001). African Literatures. Of Westerns Women and war:Angolan Ccinema and the Nation , vol.32,number 3.

Msokile, M. (1993). Misingi Ya Uhakiki wa Fasihi. Nairobi: East Africa Education Publishers.

Mugenda, O. M. (2003). Quantitative and Qualitative Approaches. Nairobi: Acts Press.

Mwangi, S. (2012). A History of constitution Making in Kenya. Nairobi: Media Development Association.

NCIC. (2013). National Integration and commission. Nairobi.

Nderitu, A. (2011). Taming the Demon of Kenya`s Election Violence. A Strategy for the NCIC .

Njagi, G. (2014). Introduction to the study of literature. Dept of Kiswahili and African Languages .

Njogu &Chimera, R. (1999). Ufundishaji wa Fasihi,Nadharia na Mbinu. Nairobi: Jomo Kenyatta Foundation.

Nyambu(Ed.), K. (2011). NCIC Training Manual. Nairobi: Ministry of justice,National Cohesion and Constitutional Affairs.

Paul.M.Juma. (2001). Mwongozo wa kiu. Nairobi: City Book Publishers.

Radhakrishan, S. (2008). Indian Philosophy. New Delhi: Oxford unniversity press.

Rossman, C. M. (2006). Designing qualitative Research 4th ed. Thousands oaks: Sage.

Scherr, A. (2013). The construction of National Identity. Migration Background-as a political and scientifically category .

Semzaba, E. (2003). Tamthilia ya Kiswahili. Dar es salaam: chuo kikuu Huria Cha Tanzania.

Smart, F. N. (2001). Research in African Literatures. Nationalism and the Aporia of National Identity in Fara`s Maps , vol.32,no.3.

Smith, A. (1993). National Identity. london: Penguin books.

SN. (26th July 2015). Nairobi: Nation media.

Stalin, J. (1913). Marxism and the National Question.

Sullivan, J. (2001). African Literatures. The Question of National Literature for Nigeria .

Thomas, G. (2009). How to do your Research Project.

Wafula, R. (1999). Uhakiki wa Tamthilia. Nairobi: Jomo kenyatta foundation.

Wamitila, K. (2008). Kanzi ya Fasihi. Nairobi: Vide Muwa.

Downloads

Published

2020-08-27

How to Cite

Mung`ala, M. J. A., Nyandoro, G. O., & Moochi, C. N. (2020). UCHUNGUZI WA UUNDAJI WA VITAMBULISHO VYA UTAIFA KATIKA TAMTHILIA YA MSTAHIKI MEYA. American Journal of Education and Practice, 4(1), 60 - 71. https://doi.org/10.47672/ajep.560

Issue

Section

Articles